AZAM FC NA SIMBA SC WAGAWANA POINTI CHAMAZI
Pambano la ligi kuu soka Tanzania bara baina ya Vinara wa ligi hiyo Simba SC na wenyeji Azam FC limemalizika kwa sare tasa ya bila kufungana mchezo mkali uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.
Simba iliyosheheni wachezaji wengi waliowahi kuitumikia Azam FC walishindwa kabisa kupenya ukuta wa safu ya ulinzi ya Azam FC ambayo ilikua Ikiongozwa na mkongwe Aggrey Morris.
Katika mchezo huo ambao ni wa kwanza baina ya timu hizo kuchezwa kwenye dimba hilo kila timu ilikua na tafadhari kubwa huku mchezo ukichezwa zaidi katikati ya uwanja .
Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kuongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 4 na magoli saba wakati Azam wa nakamura nafasi ya 3 wakiwa na pointi zao 4 na goli.
Katika mechi nyingine leo Tanzania Prisons ikiwa nyumbani ilikubali kwenda sare na Maji maji ya Songea wakifungana bao 2-2


No comments