LIVERPOOL YABUGIZWA MAGOLI YA KUTOSHA KWA MANCHESTER CITY


Wiki mbili baada ya kuibuka na ushindi mnono wa bao 4-0 dhidi ya Arsenal klabu ya Liverpool leo imejikuta ikibugizwa mabao 5-0 dhidi ya Wenyeji Manchester City katika dimba la Etihad jijini Manchester.

Mechi hiyo ya mzunguko wa nne katika ligi kuu ya soka nchini England ilishuhudia Liverpool ikimaliza mchezo huo ikiwa pungufu baada ya mshambuliaji Sadio Mane kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya kipa wa Manchester City Ederson ambaye alitolewa uwanjani akipumulia mashine baada ya tukio hilo.

Gabriel Jesus alifunga mabao mawili sawa na Leroy Sane ambaye aliingia kuchukua nafasi ya Gabriel Jesus huku Sergio Kun Aguero akifunga bao moja.

No comments

Powered by Blogger.