REAL MADRID, LIVERPOOL, MAN CITY NA SPURS ZOTE VIWANJANI LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA
Mabingwa Real Madrid wao wataanza kampeni yao ya kutaka kuvunja rekodi waliyoiweka msimu uliopita kwa kutwaa ubingwa huo kwa mara ya 3 mfululizo kama watafanikiwa kufanya hivyo tena msimu huu watakua nyumbani kumenyana na APOEL Nicosia mchezo wa kundi H.
Mchezo mwingine wa Kundi hilo ambalo linatajwa kama kundi la kifo kutokana na ubora wa timu zote zilizopo kwenye kundi hili utashuhudia Tottenham Hotspur ambayo inatumia uwanja wa Wembley kama uwanja wake wa nyumbani kutokana na matengenezo yanayofanyika kwenye uwanja wa White Hart Lane wataialika Borussia Dortmund toka Ujerumani.
Liverpool ambao wako kundi E watakua nyumbani kuialika Sevilla kutoka Spain katika mchezo ambao pengine mashabiki wanaweza kumwona Philipe Coutinho akicheza huku mashabiki wa Liverpool wakitaka kupata faraja baada ya kichapo kizito cha bao 5-0 weekend iliyopita mbele ya manchester City. Mchezo mwingine wa kundi hilo utazikutanisha Maribor watakaokua nyumbani kucheza na Spartak Moscow.
Manchester City wakiwa na usajili wa pesa nyingi upande wa ulinzi watakua ugenini kucheza dhidi ya Feyenoord ya Uholanzi wakati Shkatar Donetsk watakua nyumbani kuialika Napoli toka Italia
Kundi F lenyewe michezo miwili itachezwa usiku wa Leo Mabingwa wa zamani wa Ulaya FC Porto wataialika Besiktas ya uturuki wakati wageni katika michuano hiyo RasenBallsport Leipzing ya Ujerumani watakua wakiialika Monaco toka Ufaransa.
MECHI ZOTE HIZI ZITAANZA MAJIRA YA SAA 4 KASOROBO USIKU KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI.
No comments