CHELSEA YAWASHUSHIA MVUA YA MAGOLI "WASIOJULIKANA"


Baada ya kuikosa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu uliopita, Mabingwa wa England klabu ya Chelsea jana ilirejea kwa kishindo katika michuano hiyo mikubwa katika ngazi ya klabu ikiibuka na ushindi wa bao 6-0 nyumbani dhidi ya Qurabag ya Azerbaijan.

Mechi hiyo ilikua ni moja kati ya mechi mbili katika group C nyingine ikiwa ni ile ya AS Roma waliokua nyumbani kuwaalika Atletico Madrid ya Spain mchezo ambao ulimalizika kwa sare tasa ya bila kufungana.

Chelsea katika mchezo huo wa jana ilifanikiwa kupata magoli yote sita kupitia wachezaji tofauti goli la kwanza likifungwa na Pedro kwa shuti kali dakika ya 5 tu ya mchezo kabla ya Zappacosta hajafunga moja kati ya magoli bora usiku wa jana kwa shuti kali tokea pembeni ya uwanja baada ya kukimbia na mpira na kuwapita wachezaji kadhaa wa Qarabag FK.

Magoli mengine yalifungwa na Cisar Azpilicueta,Bakayoko, Batshuayi na goli la kujifunga la Muksim Medvedev dakika ya 82.

No comments

Powered by Blogger.