MBAPPE,NEYMAR NA CAVANI WAFUNGA PSG IKISHINDA 5, BAYERN MUNICH NAYO MAMBO SAFI


Moja kati ya mechi zilizokua zikitazamwa mno jana usiku ni PSG waliokua ugenini wakimenyana na Mabingwa wa Scotland Celtic wengi wakitaka kuona nini watakachofanya Neymar na Mbappe ambao majina yao yalikua gumzo katika usajili.

PSG kama ilivyotarajiwa na wengi imeibuka na ushindi wa bao 5-0 huku Mbappe,Neymar na Cavani wakiendelea kuonyesha umahiri wao katika si kuzisumbua beki pinzani lakini kufunga pia.

Neymar na Mbappe walifunga bao moja kila mmoja huku Edison Cavani akifunga mabao mawili na bao moja likifungwa na Michael Lusting wa Celtic akijifunga.

Mechi nyingine kwenye group hilo B wenyeji Bayern Munich wakiwa nyumbani waliifunga Anderletch ya Ubelgiji bao 3-0 magoli ya Lewandowski,Tiagho Alcantara na Joahua Kimmich.

No comments

Powered by Blogger.