BARCELONA YAIFANYIA KITU MBAYA JUVENTUS,MESSI SHUJAA
Barcelona imeanza vyema mbio za kuwania ubingwa wa Ulaya msimu huu kwa kuifunga Juventus ambao ni mabingwa wa Ulaya kwa bao 3-0.
Mchezo huo wa kundi D kwenye ligi ya mabingwa Ulaya ulichezwa nyumbani kwa Barcelona Nou Camp.
Lionel Messi ndiye aliyekua shujaa wa mchezo huo akifunga bao 2 mwenyewe huku Bao lingine likifungwa na Ivan Rakitic.
Mechi nyingine ya kundi hili ilishuhudia Olympiacos wakifungwa bao 3-2 nyumbani na Sporting Lisbon toka Ureno.

No comments