BREAKING NEWS: MBEYA CITY YAACHANA NA PHIRI

Habari Zilizotufikia Hivi Punde Zinasema Kuwa Klabu Ya Mbeya City Yenye Maskani Yake Katika Jiji La Mbeya Leo Hii Imeamua Kuvunja Mkataba Na Kocha Wake Kinnah Phiri.


Katika Taarifa Iliyotolewa Na Klabu Hiyo Kupitia Kwa Afsa Habari Wa Klabu Hiyo Ndg Shah Mjanja Haijaweka Wazi Hasa Sababu Za Mbeya City Kuvunja Mkataba Na Phiri


Kocha Phiri Alijiunga Na Mbeya City Akitokea Klabu Ya Free State Yenye Maskani Yake Huko Kwa Madiba Afrika Kusini.


Taarifa zingine zinasema kuwa kulikua na mazungumzo leo yaliyomhusisha Mkuu wa mkoa wa Mbeya mheshimiwa Makala kumlipa mshahara wa miezi sita ambao Phiri anawadai Mbeya City na bado haijaeleweka kama wamemalizana nae au vipi

Bado Tunaendelea Kumtafuta Msemaji Wa Klabu Hiyo Ili Tupate Undani Wa Suala Hili Na Tutaweletea Taarifa Kamili Ya Chanzo Cha Mkataba Huo Kuvunjwa.

No comments

Powered by Blogger.