PAULINHO AIPA USHINDI MGUMU BARCELONA, DEMBELE AUMIA
Kiungo mpya wa Barcelona Paulinho leo aliibuka shujaa wa mchezo baina ya timu yake ya Barcelona waliokua wageni wa Levante katika mechi ya ligi kuu ya Spain Maarufu kama La Liga.
Mechi hiyo ilimalizika kwa Barcelona kushinda bao 2-1 licha ya kutangulia kufungwa dakika ya 39 kwa goli safi kabisa la Gabu Shibasaki bao ambalo lilidumu mpaka dakika ya 62 wakati Dennis Suarez anaisawazishia Barcelona.
Kiungo Paulinho aliifungia Barcelona bao la ushindi dakika ya 84 ikiwa ni dakika 7 tu tangu alipoingia uwanjani kuchukua nafasi ya Ivan Rakitic.
Barcelona katika mechi hiyo ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake mpya Ousmane Dembele kuumia dakika ya 29 tu ya mchezo kwa kile kilichoonekana kama Maumivu ya misuli ya paja.

No comments