YANGA YAVUTWA SHATI NA MAJI MAJI SONGEA
Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Majimaji ambao walikua wenyeji wa Yanga katika uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo timu hizo zimetoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.
Mchezo ulikua mgumu hasa kipindi cha kwanza ambapo milango ilikua migumu kutokana na timu zote kutoruhusu mashambulizi katika maeneo yao ya hatari.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Majimaji waliochagizwa na ingizo la Jerison Tegete na Abdulhalim Humoud wakiwa wa kwanza kupata bao lililofungwa katika dakika ya 54 na Peter Mapunda.
Yanga waliamka baada ya bao hilo na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha katika dakika ya 79 lililofungwa na Donald Ngoma kwa kichwa akiunganisha krosi ya Obrey Chirwa.
Hadi dakika 90 zinakamilika, Majimaji 1-1 Yanga.
Matokeo mengine ya ligi hiyo katika michezo mbalimbali ni kama ifuatavyo;
Stand 0-1 Singida
Prisons 0-0 Ndanda
Lipuli 0-0 Ruvu Shooting
Mtibwa 2-1 Mbao FC

No comments