EPL LEO: AGUERO APIGA HAT-TRICK MAN CITY IKIUA 6, LIVERPOOL NA SPURS ZAPUNGUZWA KASI


Mzunguko wa 5 katika ligi kuu ya Soka Nchini England uliendelea leo kwa mechi 7 kuchezwa kwenye viwanja tofauti nchini Humo.

Habari kuu ya Siku ikawa ni matokeo ya bao 6-0 waliyopata Manchester City ugenini dhidi ya Watford huku Sergio Aguero akifunga mabao matatu kwenye ushindi huo mnono mabao mengine yakifungwa na Raheem Sterling,Otamendi na Gabriel Jesus.

Liverpool ikiwa nyumbani ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Barnley Scott Aifield akutangulia kuipatia Burnley bao la kuongoza kabla ya Mohamed Salah hajaisawazishia Liverpool dakika 3 badae.

Tottenhm ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani ilishindwa kupata pointi zote tatu dhidi ya Swansea wakitoka sare ya bila kufungana.

Newcastle wakiwa nyumbani waliifunga Stoke City bao 2-1 wakati Crystal Palace ikilazwa bao 1-0 na Southampton.

Huddersfield town ikalazimishwa sare ya bao 1-1 na Leicester City wakati West Brom na West Ham nao wakitoka sare ya bila kufungana.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mechi mbili kuchezwa Man United wakiikaribisha Everton wakati Chelsea wataialika Arsenal.

No comments

Powered by Blogger.