NOMA: DE GEA AFIKISHA MECHI 100 BILA KUFUNGWA
Ushindi wa bao 4-0 walioupata Manchester United juzi dhidi ya Everton umemfanya kipa wa timu hiyo David de Gea kufikisha mechi 100 bila kufungwa (Clean sheets) akiwa na Man United.
Tangu ajiunge na Manchester United akitokea Atletico Madrid David De Gea amekua muhimili mkuu wa klabu hiyo katika nafasi ya kipa akichukua nafasi ya Edwin Van Der Sar aliyestaafu.
Katika mechi hizo 100 bila kufungwa De Gea hajafungwa katika mechi 80 za Ligi kuu ya England, Mechi 10 za ligi ya mabingwa Ulaya, Mechi 5 za Kombe la Ligi EFL, Mechi 4 za Kombe la FA na mechi 1 ya Europa League.

No comments