MESSI APIGA NNE, ZAZA APIGA TATU BARCELONA NA VALENCIA ZIKIGAWA DOZI LA LIGA

Barcelona 6-1 Eibar: Lionel Messi bags a hat-trick
Jumla ya magoli 12 Yalifungwa katika mechi mbili za ligi kuu ya Spain maarufu kama La Liga Santander huku Lionel Messi na Simon Zaza wakifunga zaidi ya 50% ya magoli hayo.

Valencia wakiwa nyumbani walifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa bao 5-0 dhidi ya Malaga kwenye mchezo wa kwanza ambao mpaka mapumziko Valencia walikua mbele kwa bao 1-0.

Mshambuliaji wa zamani wa West Ham na Juventus Simon Zaza alifunga mabao matatu (hat-trick) kwenye mechi hiyo ambayo Rodrigo na Santi Mina nao walifunga kwa upande wa Valencia.

Kwenye mechi ya pili hiyo jana Barcelona wakiwa nyumbani waliifunga Eibar bao 6-1 shujaa wa mchezo si mwingine bali ni mchawi wa soka Lionel Messi ambaye alifunga bao 4 katika mchezo huo ambao nao mpaka mapumziko Barcelona walikua mbele kwa bao 2-0 bao moja lilifungwa kwa njia ya penati na Lionel Messi baada ya beki wa pembeni Semedo kuangushwa katika eneo la hatari na lingine likifungwa na Paulinho.

Kipindi cha pili Messi aliongeza mabao mengine matatu huku Dennis Suarez akifunga naye bao 1 na kuihakikishia Barcelona ushindi ambao unazidi kuwaweka kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa hawajapoteza mechi yoyote mpaka sasa wakijikusanyia pointi 15 baada ya michezo mitano.

No comments

Powered by Blogger.