ADHABU IMEISHA SASA RONALDO RUKSA KUREJEA DIMBANI KESHO
Baada ya kutumikia adhabu ya mechi 5 nje ya Uwanja Ronaldo anatarajia kurejea dimbani kesho Jumatano dhidi ya Real Betis katika mechi ya la Liga pale Bernabeu.
Ronaldo alifungiwa kucheza mechi 5 kufuatia kumsukuma mwamuzi katika mchezo wa kwanza wa mechi ya Spanish super Cup dhidi ya Barcelona.
Amekosa kuichezea Real Madrid katika mechi kadhaa zikiwemo dhidi ya Barcelona ambayo ilikua ni mechi ya marudiano na mechi 4 za Ufunguzi dhidi ya Deportivo La Coruna,Valencia, Levante na Real Sociedad
kurudi kwa Ronaldo ambaye wiki iliyopita aliichezea Real Madrid kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kufunga magoli mawili itakua ni ahueni kwa kocha Zinadine Zidane baada ya Karim Benzema Kuumia hivyo kulazimika kumtumia chipukizi Borja Mayoral.
mechi ya kesho itakua ndiyo ya kwanza kwa Ronaldo msimu huu wa La Liga akitaka kuendeleza rekodi ya kufumania nyavu n kuisaidia Real Madrid kushinda mataji
No comments