NIYONZIMA FITI KUPAA NA MNYAMA KUWAFATA MBAO

Kiungo Haruna Niyonzima wa Simba atasafiri na wachezaji wenzake kesho kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC baada ya kupona maralia.

Niyonzima alikosa mchezo wa jana  dhidi ya Mwadui FC katika uwanja wa Uhuru ambapo Wekundu hao waliibuka na Ushindi wa mabao 3-0.

Mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba, Hajji Sunday Manara amesema  Mnyarwanda huyo hali yake  imeimarika na atakuwa miongoni wa nyota watakaosafiri kuelekea jijini humo.

"Niyonzima yuko fiti kesho atasafiri na wenzanke kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mbao FC keshokutwa Alhamisi," alisema Manara.

Manara Amesema Uongozi wa Simba hauna  sababu ya kuachana na kocha wake Joseph Omog na watu wanaodhani kuwa Mcameroon huyo atatimuliwa waandike wameumia.

"Uongozi wa Simba hauna sababu ya kuachana na kocha Joseph Omog. Ni kocha Mzuri na ameisaidia Simba Kufanya Vizuri mpaka sasa," alisema Manara.

No comments

Powered by Blogger.