BAADA YA KUSHINDWA KUPATA POINTI YOYOTE LIGI KUU, KOCHA NJOMBE MJI AJIUZULU.

Kocha mkuu wa Timu ngeni ligi kuu ya soka Tanzania bara Timu ya Njombe Mji ndugu Ahmed Hassani Banyai amebwaga manyanga kuifundisha timu hiyo.

Banyai amefikia uamuzi huo yeye mwenyewe baada ya kuona Ameshindwa kupata matokeo katika mechi zote za ligi kuu msimu huu ambapo mpaka sasa mechi 3 zimeshachezwa.

Njombe Mji ilianza ligi kwa kupoteza mechi yake ya kwanza dhidi ya Tanzania Prisons kisha ikapoteza 1-0 dhidi ya Yanga na jana ikipoteza tena ugenini bao 1-0 mbele ya wenyeji Mbeya City.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya habari ya klabu hiyo inasema kwasasa timu hiyo itakua chini ya kocha msaidizi Mrage Kabange baada ya kupokea barua rasmi toka kwa kocha Banyai huku mchakato wa kumpata kocha mpya ukianza mara moja.

Njombe Mji na Stand United ndiyo timu pekee katika msimamo wa ligi kuu ya Vodacom ambazo hazijapata pointi yoyote mpaka sasa huku Mtibwa wakiwa ndiyo vinara baada ya kishinda mechi zote 3.

No comments

Powered by Blogger.