BENCHI LA UFUNDI LA YANGA LAHAMIA MAHAKAMANI KISUTU KWA MUDA
Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina leo aliliongoza benchi la ufundi la klabu hiyo lilipofika katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumpa 'kampani' aliyekua mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji.
Manji anayekabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya alifika mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo ambayo hata hivyo imehairishwa baada ya mshtakiwa, Yusuf Manji kuchelewa kufika mahakamani hapo kwa madai ya kwamba alipitia hospitali kwa ajili ya matibabu.
Katika viwanja vya mahakama, Lwandamina akiwa na kocha msaidizi wa Yanga Shadrack Nsajigwa, kocha wa makipa Juma Pondamali na meneja Hafidh Saleh walionekana wakiteta wakisalimiana na Manji na kuteta mawili matatu huku mfanyabiashara huyo akitumia muda mwingi kuzungumza na nahodha wa Yanga Nadir Haroub ambaye ambaye naye alikuwepo katika msafara huo.
Kwa miaka kadhaa, Yusuf Manji amekua msaada mkubwa sana kwa Yanga kiuchumi tangu akiwa mfadhili wa klabu hiyo hadi alipoamua kuwa mwenyekiti hali iliyosababisha mambo kwenda mrama katika klabu hiyo pale mfanyabiashara huyo alipopata matatizo ya kimahakama yaliyomyumbisha kiuchumi.

No comments