PLUIJM SASA RUKSA KUKAA KATIKA BENCHI SINGIDA UNITED
Kocha mkuu wa Singida United, Mholanzi Hans Van Pluijm amemaliza adhabu yake ambayo imemweka nje ya michezo mitatu ya ligi kuu.
Pluijm alikumbwa na adhabu hiyo kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu alivyovionesha Mwezi Novemba mwaka jana katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.
Sasa Pluijm yupo tayari kukaa katika benchi la timu yake kwa mara ya kwanza tangu msimu mpya wa ligi kuu ulipoanza.
“Nashukuru nimemaliza adhabu yangu na nitaanza kukaa katika benchi kwenye mechi yetu dhidi ya Kagera Sugar, kwa ufupi kikosi changu hakijaanza vibaya msimu huu japo wachezaji wangu wengi si wazoefu na ligi kuu. Alisema Hans
Hans aliongeza kuwa kwa sasa bado anaendelea na kazi ya kukisuka kikosi chake.
“Kazi kubwa ambayo ninayo sasa ni kuwapa uzoefu wachezaji wangu kwani wengi si wazoefu wa ligi hii, nimekuwa hapa kwa muda mrefu na najua ligi ni ngumu, hivyo ni lazima tupambane kwa hali yoyote ile kwenye maandalizi yetu ili kutoa ushindani wa kweli kwa wapinzani wetu,

No comments