NITENDELEA KUPAMBANA KWA AJILI YA HII TIMU - PHILIPPE COUTINHO


Uamisho wake wa kwenda Barcelona ulizungumzwa sana na vyombo vya habari za michezo duniani kote, vijiwe vya soka vilijadili sana juu ya uhamisho huu, kule kukaa kwake kimya ndiyo kukawaamisha wengi kuwa sasa Liverpool ijiandae na maisha bila fundi huyu wa kibrazil hasa ukizingatia kuwa timu inayomtaka ni Barcelona.


Lakini kwa kuwa liverpool walimuhitaji zaidi wakaamua kuwawekea ngumu mpaka dakika ya mwisho na kukataa kwauzia Barcelona silaha hii. Ukimuulize Mwenyewe anakwambia alipenda sana kwenda Barcelona lakini ndiyo hivyo haikuwezekana.

lakini sasa hayo ni kama yamekwishwa kwake muda na sasa yuko tayari kuitumikia Liverpool kwa zaidi ya asilimia 100. Huyu si mwingine bali ni Philippe Coutinho Correira Fundi wa Kibrazil mwenye miaka 25ambaye yuko tayari kurudisha ile imani kwa Liverpool.

Alipoulizwa kuhusu Saga la Uhamisho wake alisema "Niko pouwa kwa sasa, hayo yote yalishapita, kwa sasa nahitaji kupambana kwa nguvu na uwezo wangu wote kwa ajili ya Liverpool" alimaliza Coutinho.

No comments

Powered by Blogger.