BAADA YA KIPIGO CHA PSG, BAYERN MUNICH YAMTIMUA KOCHA CARLO ANCELOTT
Habari kutoka katika vyanzo mbalimbali vya habari Nchini Ujerumani na barani Ulaya vimeeleza kuwa Klabu ya Bayern Munich Imeamua kumvungia virago kocha wake Carlo Ancellot
Hiyo inakuja masaa machache baada ya mabingwa hao wa Ujerumani kufungwa bao 3-0 na Paris Saint German ya Ufaransa katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya
Kocha huyo Raia wa Italia amedumu na Bayern Munich kwa miezi 15 pekee na ataiacha Bayern ikiwa katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga.
No comments