RUNGU LA TFF LAMUANGUKIA PLUIJM
Kamati ya bodi ya uendeshaji na usimamizi wa ligi kuu ya Vodacom na ligi daraja la kwanza, maarufu kama kamati ya saa 72 imemuadhibu kocha wa Singida United Kocha wa timu ya Singida United, Hans van der Pluijm kwa kumtoza faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuingia katika vyumba vya wachezaji na kutoa maelekezo wakati akiwa anatumikia adhabu ya kukosa mechi tatu aliyopata msimu uliopita akiwa na timu ya Yanga.
Adhabu dhidi ya Kocha Pluijm imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 40(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.
Mmiliki wa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga ameandikiwa barua kwa uwanja huo kukosa maji ya bomba na badala yake kutumia maji ya kwenye ndoo au madumu hali hiyo ambayo inahatarisha afya za wachezaji.

No comments