LIGI KUU YA ENGLAND: LACAZETTE AIPA ARSENAL USHINDI MUHIMU NYUMBANI

Arsenal 2-0 West Brom: Alexandre Lacazette at the double
Mshambuliaji mpya wa Arsenal Mfaransa Alexandre Lacazette jana usiku aliibuka shujaa kwa timu yake akifunga mabao yote mawili katika ushindi wa bao 2-0 walioupata Arsenal nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion.
Mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Alexis Sanchez uliokolewa na kipa wa West Brom Ben Foster kisha kugonga mwamba na kurudi uwanjani na ndipo ulipomkuta Lacazette aliyefunga kwa kichwa bao la kwanza ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Lacazette aliipatia Arsenal Bao la pili kwa njia ya penati baada ya Aaron Ramsey kuangushwa katika eneo la hatari na mwamuzi kuamuru kupigwa penati na Lacazette akachukua jukumu hilo kufunga bao lake la pili lililowapa Arsenal ushindi muhimu ambao unawatoa katika nafasi ya 12 mpaka nafasi ya 7.

Ligi hiyo itaendelea tena weekend hii inayokuja kisha itasimama mpaka tarehe 14 Oktoba kupisha mechi za timu za taifa 

No comments

Powered by Blogger.