DORTMUND KUWAKARIBISHA REAL MADRID, MAN CITY NA SHAKTAR RATIBA MABINGWA ULAYA LEO JUMANNE
Ligi ya Mabingwa Ulaya inaingia kwenye mzunguko wake wa pili leo katika hatua ya Makundi ya Ligi hiyo kubwa kwa upande wa klabu ambayo pia inavipa vilabu pesa nyingi barani Ulaya.
Makundi manne ya ligi hiyo itashuhudia mechi mbili kila kundi zikichezwa katika viwanja vinane barani humo
Mabingwa watetezi Real Madrid wao watakua ugenini baada ya kupata ushindi kwenye mechi yao ya kwanza safari hii wakiivaa Borussia Dortmund ya Ujerumani katika mechi za kundi H kundi ambalo linaonekana ni kundi la Kifo huku Tottenham Hotspur ambao walianza na ushindi dhidi ya Borussia Dortmund watasafiri mpaka Cyprus kuivaa APOEL Nicosia.
Manchester City ambayo msimu huu imeanza vyema kwa kupata ushindi mnono katika mechi zao watakua nyumbani kuialika Shaktar Donetsk ya Ukraine wakati Napoli atacheza dhidi ya Feyernoord ya Uholanzi katika mechi za kundi F.
Mabingwa wa Uturuki Besiktas baada ya kupata ushindi muhimu ugenini dhidi ya FC Porto safari hii watakua nyumbani kucheza dhidi ya wawakilishi wa Ujerumani RasenBallsport Leipzig wakati Monaco wataialika FC Porto katika mechi mbili za kundi G.
Liverpool wao wamesafiri kilometa zaidi ya 2000 kuwavaa Spartak Moscow ya Russia wakati Sevilla wataialika Maribor FC ya Slovenia katika mechi za kundi E.
RATIBA YA MECHI HIZI ZOTE NI SAA NNE KASOROBO USIKU KWA SAA ZA AFRIKA MASHARIKI
No comments