HIKI NDICHO KILICHOTOKEA USIKU WA JANA KATIKA LIGI YA MABINGWA ULAYA
Hatua ya kwanza ya mechi za makundi katika ligi ya mabingwa barani Ulaya zilichezwa jana ikiwa ni mwendelezo wa mechi zilizoanza kuchezwa siku ya jumanne na kushuhudiwa hiyo jana jumla ya magoli 26 yakifungwa kwenye michezo minane.
Harry Kane wa Tottenham Hotspur na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid wote walikua mashujaa kwa kuongoza kwenye mbio za kushika tuzo ya mfungaji bora kila mmoja akifunga mabao mawili kwenye michezo yao. Real Madrid wakiifunga Apoel Nicosia bao 3-0 huku Tottenham ikiiadhibu borussia Dortmund bao 3-1 zikiwa ni mechi za kundi H kundi ambalo linaonekana kuwa ni gumu mno,
Liverpool wakiwa Nyumbani Anfield walilazimishwa sare ya bao 2-2 na Sevilla kutoka Spain pambano kali ambalo Liverpool walipata mabao yao kupitia kwa Mohamed Salah na Roberto Firminho katika mechi hiyo ya kundi E ambapo mechi nyingine ilishuhudiwa Maribor wakitoka sare ya bao 1-1 na Spartak Moscow.
Kundi F nalo mechi mbili zilichezwa hiyo jana Fayeernord ikiwa nyumbani ilifungwa bao 4-0 na kikosi cha kocha Pep Guadiola magoli ya Sergio Aguero, Gabriel Jesus na mlinzi John Stones aliyefunga mabao mawili huku mechi nyingine ya kundi hilo Shaktar Donetsk ikiwalaza napoli bao 2-1
Kundi G Klabu ya FC Porto ikiwa nyumbani ilifungwa bao 3-1 na besiktas ya Uturuki wakati RB Leizpig ya ujerumani ikitoshana nguvu na mabingwa wa Ufaransa Monaco wakifungana bao 1-1.
No comments