RONALDO AREJEA NA KUPIGA BAO 2, REAL MADRID IKIANZA KUTETEA UBINGWA
Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo jana alirejea dimbani wakati klabu yake ya Real Madrid ikianza kutetea ubingwa wao wa ligi ya mabingwa Barani Ulaya akifunga bao 2 katika ushindi wa bao 3-0 walioupata kwenye mechi yao ya kwanza dhidi ya APOEl Nicosia ya Cyprus.
Ronaldo ambaye amefungiwa kuichezea Real Madrid kwenye mechi za ndani ya Spain alianza mchezo wa jana na kufanikiwa kupata bao pekee kwenye kipindi cha kwanza dakika ya 12 tu akiunganisha mpira wa krosi wa Gareth Bale kutoka upande wa kushoto wa uwanja bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha Pili Real Madrid ambao wako katika Group H waliendelea kulisakama lango la Apoel na kufanikiwa kupata mabao mengine mawili bao la pili likifungwa na Ronaldo kwa njia ya penati baada ya beki wa Apoel kuunawa mpira kwenye eneo la hatari na goli la tatu lilifungwa na nahodha Sergio Ramos akiunganisha mpira wa kichwa wa Gareth Bale.
No comments