EPL LEO: CHELSEA NA ARSENAL HAKUNA MBABE,DAVID LUIZ ALIMWA KADI NYEKUNDU
Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini England Chelsea leo wameshindwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani kwa kwenda sare ya bila kufungana na Arsenal.
Mchezo huo uliopigwa "darajani" ulimalizika kwa sare tasa ya bila kufungana licha ya kosa kosa kwa pande zote mbili.
Katika mechi hiyo Chelsea wamempoteza beki wake David Luiz aliyepata kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mlinzi wa Arsenal Sead Kolasinac.
Matokeo hayo yanawafanya Chelsea kufikisha pointi 10 huku Arsenal wakifikisha pointi 7.

No comments