OKWI HATARI MECHI MBILI GOLI 6 SIMBA IKIENDELEZA USHINDI BILA KUFUNGWA GOLI


Mchezaji bora wa mwezi wa nane kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara Emmanuel Okwi wa Simba ameendeleza kasi yake ya kuzifumania nyavu akifunga mabao mawili leo katika ushindi wa bao 3-0 walioupata Simba dhidi ya Mwadui.

Ikicheza katika dimba la Uhuru jijini Dar Es Salaam Simba ambao walikua wenyeji wa mchezo huo iliwachukua dakika 7 tu kupata bao la kuongoza likifungwa na Emmanuel Okwi bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili mnamo dakika ya 67 Emmanuel Okwi tena aliwanyanyua Mashabiki wa Simba akifunga bao la pili baada ya kuwahadaa mabeki wa mwadui waliodhani anapiga moja kwa moja kumbe alikua anatishia kisha kumchungulia kipa na kupiga kiufundi na bila ajizi mpira ulizama nyavuni.

John Bocco maarufu kama Adebayor ndiye aliyefunga ukurasa wa mabao kwa Simba akifunga bao la tatu na la mwisho na kuwafanya Simba sasa kufikisha pointi 7 wakiwa na magoli 10 baada ya mechi 3.

Katika mechi nyingine ya ligi hiyo leo Wenyeji Mbeya City waliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Njombe Mji mchezo uliochezwa kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya.

No comments

Powered by Blogger.