ROONEY AKUMBANA NA KICHAPO CHA NGUVU AKIREJEA OLD TRAFFORD
Mfungaji bora wa muda wote wa Manchester United na mshambuliaji wa sasa wa klabu ya Everton Wayne Rooney jioni ya leo alirejea Old Trafford kucheza dhidi ya Klabu yake hiyo ya zamani.
Manchester United iliibuka na ushindi wa bao 4-0 katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford.
Antonio Valencia alifungua akaunti ya mabao kwa kufunga bao la kwanza kwa shuti kali likiwa moja kati ya magoli bora kabisa kiwahi kufungwa katika ligi kuu ya England bao ambalo lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili hasa kuanzia dakika ya 80 ilikua chungu kwa kikosi cha kocha Ronald Koeman kwani Beki ya Everton iliweza kuruhusu mabao matatu yakifungwa na Henrik Mkhtaryan,Romelu Lukaku na Antony Martial.
Wayne Rooney alitoka mnamo dakika ya 82 na nafasi yake kuchukuliwa na Kevin Mirallas huku uwanja mzima ukisimama kumpigia makofi shujaa huyu.
Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kulingana kwa kila kitu na majirani zao Manchester City zote zikiwa na pointi 13 wakati Hali ni mbaya kwa Everton ambao wamejikusanyia pointi 4 mpaka sasa na wanashika nafasi ya 18.

No comments