VICENT BOSSOU KUISHITAKI YANGA FIFA


Beki wa zamani wa Yanga, raia wa Togo Vincent Bossou ametishia kuiburuza klabu yake hiyo ya zamani katika shirikisho la soka duniani, FIFA akilalamikia madai ya mishahara yake ya miezi miwili.

Beki huyo ambaye ameondoka Yanga kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika amesema atawatumia Yanga barua ya mwisho ya madai yake na iwapo wataendelea kumpuuza basi wakala wake atachukua hatua.

Kwa upande wa wakala wa mchezaji huyo, mganda Gibby Kalule, amesema amekua akiwasiliana na uongozi wa Yanga mara kadhaa kuhusu deni lao lakini viongozi hao wamekua hawajibu e-mails wala kupokea simu zake hivyo iwapo wataendelea hivyo watapeleka malalamiko FIFA.

No comments

Powered by Blogger.