MSIMU MPYA BUNDESLIGA KUANZA LEO,MABINGWA BAYERN MUNICH UWANJANI
Msimu mpya wa ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga unaanza leo Ijumaa kwa pambano moja katika uwanja wa Alianz Arena baina ya Wenyeji Bayern Munich ambao ni mabingwa watetezi dhidi ya Bayer Leverkusen.
Mchezo huo utakaoanza majira ya saa 3 na nusu za usiku kwa saa za hapa nyumbani Afrika Mashariki.
Bayern Munich ambayo haikufanya vyema kwenye michezo ya kujipima nguvu itakua na mtihani wa kwanza mbele ya mashabiki wake kutaka kuwaonyesha nini wakitegemee kwenye kikosi cha kocha Carlo Ancellot.
No comments