TSHISIMBI WA YANGA AWASILI NA KWENDA MOJA KWA MOJA KAMBINI PEMBA
Kiungo huyo kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland alisaini mkataba wa miaka miwili na yanga hivi karibuni lakini inaelezwa kwamba alikua na tatizo katika passport yake ambalo lilikua likishughulikiwa.
Kuwasili kwa kiungo huyo mkabaji kunashusha presha za mashabiki wa Yanga ambao walikua wakimsubiri kwa hamu nyota huyo, hasa wakati huu ambao wanajiandaa kuwakabili watani zao wa jadi.
No comments