MBARAKA YUSUF SASA RUKSA KUKIPIGA AZAM FC
Klabu ya Azam FC imesema tayari imemalizana na Kagera Sugar kuhusu sakata la usajili wa mchezaji Mbaraka Yusuf.
Mbaraka ambaye alijiunga na wanalambalamba mnamo June mwaka huu akitokea Kagera Sugar aliwekewa pingamizi na klabu yake hiyo ya zamani kwa madai kwamba alikua bado na mkataba nao.
Taarifa ya afisa habari wa Azam FC, Jafar Iddi inasema kwamba jana walikua na kikao na Kagera Sugar na wamekubaliana na wanankurukumbi. Sasa Mbaraka yupo huru kuitumikia Azam FC katika msimu ujao.
Katika makubaliano hayo, Kagera Sugar wamekubali kutoa barua ya kumruhusu Mbaraka kuichezea Azam bila kikwazo cha aina yoyote.
No comments