BARCELONA WAMKOMALIA COUTINHO WAONGEZA PESA KUWARIDHISHA LIVERPOOL
Katika hali inayoonekana wamedhamiria Barcelona wameongeza dau la fedha kutaka kuwashawishi Liverpool wamruhusu Philip Coutinho kujiunga nao.
Habari zilizotoka jioni hii zinasema kwamba Barcelona wamepeleka dau la Euro 120M kutoka kwenye dau la Euro 100M lililoripotiwa awali fedha ambazo wataalamu wa mambo wanaona kabisa Liverpool hawatakua na ubavu wa kukataa.
Barcelona wanahaha sasa kuimarisha timu yao baada ya kuondoka Neymar na tayari Phili Coutinho na Osmane Dembele wa Borussia Dortmund wanatajwa kuweza kutimkia Barcelona lakini makubaliano hayajafikiwa mpaka sasa.
Mapema wiki hii kocha mkuu wa Liverpool Juggen Klopp alirudia kauli yake kwamba Coutinho hauzwi.
No comments