HAZARD NA BAKAYOKO WAKO TAYARI KUIVAA TOTTENHAM (+PICHA)


Majeruhi katika kikosi cha Chelsea ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya England wameendeelea kupungua baada ya Mshambuliaji Eden Hazard na kiungo Timoue Bakayoko kurejea kikosini tayari kwaajili ya mchezo wa Weekend hii dhidi ya Tottenham.

Habari ya kurejea kwa wachezaji hao ni faraja sio tu kwa kocha Antonio Conte lakini pia kwa mashabiki wa Chelsea duniani kote baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Burnley Nyumbani.

Hazard na Bakayoko walicheza mchezo wa kirafiki jana dhidi ya QPR na Chelsea kushinda bao 8-0 ikiwa ni moja ya maandalizi ya mechi yao dhidi ya Tottenham ambayo itachezwa kwenye dimba la Wembley ambao ni uwanja wa nyumbani wa Tottenham wakati huu ambao wanakarabati uwanja wao.


No comments

Powered by Blogger.