NEYMAR AFANYIWA VIPIMO TAYRI KUVUNJA REKODI YA UHAMISHO KUELEKEA PSG
Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya Taifa ya Brazil Neymar jana alikuwa nchini Ureno akifanyiwa vipimo vya afya tayari kwaajili ya uhamisho utakaotoa rekodi mpya ya fedha kwenda PSG ya Ufaransa.
Ndege maalumu ilimpeleka Neymar mjini Porto kwaajili ya Vipimo huku kukiwa na usiri mkubwa juu ya uhamisho wa nyota huyu mwenye mia 25 tu si kwa Barcelona wala PSG ambao wameshatoa tamko rasmi kuhusu kuondoka au kuwasili kwa Neymar japokua taarifa za jana zilieleza kwamba Barcelona wamesema Neymar anataka kuondoka klabu ni hapo.
Rafiki mkubwa wa Neymar kwenye kikosi cha Barcelona Lionel Messi jana hiyo hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka video inayomuonyesha jinsi alivyokua karibu na Neymar na kumtakia maisha mema huko aendako.
Inasemekana leo Alhamis Neymar atakua jijini Paris tayari kwaajili ya Utambulisho na kukamilisha baadhi ya mambo kwenye mkataba wake ambao unatajwa kuwa ni mkubwa kuwahi kutokea Duniani ikiwa ni paundi milioni 198 kama Usajili pamoja na mshahara wa 596,000 kwa wiki baada ya kodi akitarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano ambavyo kwa pamoja vitaigharimu PSG takribani paundi milioni 398 mpaka mkataba wake utakapoisha.
Uhamisho wa Neymar unaenda kuvunja rekodi ya paundi milioni 89 waliyotoa Manchester United kumsajili Paul Pogba
No comments