MIZINGA YA RUVU SHOOTING YAILIPUA YANGA CHAMAZI
Mabingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga wamekumbana na kichapo cha bao 1-0 toka kwa maafande wa Ruvu Shooting toka Pwani
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam lilikua ni mahususi kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara baadae mwezi huu.
Goli pekee la Ruvu Shooting lilifungwa kipindi cha kwanza likiwa ni goli la kujifunga la beki mpya wa Yanga Abdallah Haji Shaibu maarufu kama Ninja Wakati akijaribu kuokoa mpira wa krosi ya moja kati ya washambuliaji wa Ruvu Shooting.
Yanga baada ya mchezo huo itaelekea Zanzibar kujiandaa na mechi dhidi ya Simba tarehe 23 mwezi huu jijini Dar es Salaam.
No comments