LICHA YA ZENGWE LA URAIA, KARIA AIBUKA MSHINDI URAISI TFF,WAMBURA MAKAMU
![]() |
Rais wa T.F.F Wallace Karia |
Walace Karia ambaye aliwekewa pingamizi wakati wa mchakato wa uchaguzi huo kwamba sio Raia wa Tanzania na hatimaye Uhamiaji kuja kuthibitisha uraia wake ameshinda kwa jumla ya kura 95 za wajumbe wa mkutano huo mkuu wa TFF.
Sambamba na Karia pia Wajumbe wa Mkutano mkuu wamemchagua Michael Wambura kuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne toka sasa.
Habari kuhusu wajumbe walioshinda tutazidi kuwaletea endelea kutufatilia.
No comments