MABINGWA CHELSEA WAANZA LIGI KWA KICHAPO, ROONEY AIBEBA EVERTON


Unaweza kusema imekua siku mbaya kwa Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Chelsea baada ya kukumbana na kichapo cha bao 3-2 katika mchezo wao wa ufunguzi dhidi ya Burnley kwenye dimba lao la nyumbani Stamford Bridge

Licha ya kufungwa bao hizo lakini pia imejikuta ikiwapoteza nyotavwake wawili ambao ni nahodha Gary Cahil na kiungo Cesc Fabregas baada ya kupata kadi nyekundu, Cahill akipata kadi ya moja kwa moja nyekundu wakati Fabregas yeye alipata kadi mbili za njano.

Everton ikiwa nyumbani iliwalaza Stoke City bao 1-0 bao pekee la Mshambuliaji Wayne Rooney ambaye amecheza mechi yake ya kwanza kwenye ligi akiwa na klabu hiyo tangu alipojiunga nayo msimu huu akitokea Manchester United.

Crystal Palace walishangazwa nyumbani baada ya kufungwa na timu ngeni iliyopanda daraja ya Huddersfied kwa kufungwa bao 3-0 Ukiwa ni mchezo wa kwanza katika ligi kwa Kocha mpya Frank De Boer.

Swansea City ikisafiri mpaka Southampton ilishindwa kupata ushindi ikilazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji Southampton ikiwa  mechi pekee ya ufunguzi mpaka sasa ambapo imeisha bila magoli kufungwa.

West Brom ikiwa nyumbani iliifunga Bournemouth bao 1-0 wakati mchezo wa utangulizi leo majira ya saa 8 mchana  Watford walienda sare ya bao 3-3.

Manchester City ambayo inapewa nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa msimu huu iliibuka na ushindi wa bao 2-0 magoli yà Sergio Aguero na goli la kujifunga la Lewis Dunk dhidi ya Wageniklabu ya Brighton & Hove albioni.

Ligi inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezo miwili miwili kuchezwa.




No comments

Powered by Blogger.