LIVERPOOL YAANZA LIGI KUU YA ENGLAND KWA SARE


Liverpool wameanza msimu mpya wa ligi kuu ya soka nchini England kwa mwaka 2017/2018 kwa sare ya bao 3-3 ugenini dhidi ya Watford.

Liverpool walianza mchezo huo Kwa kusuasua na kujikuta wakifungwa bao la kwanza dakika ya 8 tu likifungwa na Stefano Kaka Chuka lakini mshambuliaji wa liverpool Sadio Mane aliisawazishia Liverpool bao hilo dakika ya 29 kabla ya Abdoulaye Doucoure kuiongezea Watford bao la pili dakika mbili baadae na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko Watford wakiwa mbele kwa bao 2-1

Kipindi cha pili Liverpool walizinduka na kupata mabao ya haraka kupitia kwa Roberto Firminho na Mohamed Salah lakini wakashindwa kulinda mabao hayo na kukubali Watford kusawazisha dakika za mwisho kupitia kwa Miguel Bristos na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 3-3.

Mechi nyingine zinaendelea muda huu

No comments

Powered by Blogger.