COUTINHO APELEKA OMBI RASMI LA KUTAKA KUONDOKA LIVERPOOL
Ikiwa ni siku ya kwanza leo kwa msimu mpya wa ligi kuu ya England kuchezwa taarifa zimeeleza kwamba Mshmbuliaji wa Liverpool Philip Coutinho amewasilisha ombi rasmi la kutaka kupata ruhusa ya kuondoka na kujiunga na Barcelona.
Hii inakuja masaa machache baada ya Kocha mkuu wa timu hiyo Juggen Klopp kutanabaisha kwamba mchezaji huyo hatouzwa kwa kiasi chochote cha pesa huku taarifa zikisema kwamba Paundi milioni 90 zilizopelekwa na Barcelona zimekataliwa
Pengine hatua hii ya mchezaji mwenyewe kutaka kuondoka sasa itawaamsha kivingine mabosi wa Liverpool na kufikiria mara nyingine jinsi gani watamlazimisha mchezaji ambaye tayari ametaka kuondoka.
Liverpool itasafiri kuivaa Watford kesho kwenye mchezo wake wa ufunguzi huku Coutinho akikosekana kwenye kikosi kitakachocheza kesho kutokana na kile kinachoelezwa kwamba ana majeraha madogo aliyoyapata wakati wa mazoezi.
JE UNADHANI LIVERPOOL WATAMRUHUSU COUTINHO KUONDOKA?
No comments