ARSENAL YAKUBALI KUMFANYA SANCHEZ MCHEZAJI ANAYELIPWA PESA NYINGI ZAIDI EPL ILI ABAKI
Sakata la kumwongezea Mkataba mshambuliaji Alexis Sanchez wa Arsenal limeingia hatua nyingine ambapo sasa klabu hiyo ambayo ndiyo mabingwa wa kombe la FA kuamua kukubali matakwa ya mchezaji huyo ili asaini mkataba mpya.
Alexis Sanchez mwenye miaka 28 ameingia katika mgogoro na klabu yake ya Arsenal siku za hivi karibuni akikataa mshahara wa paundi 225,000 aliokua ameahidiwa kama angekubali kusaini mkataba mpya na kusema anataka si chini ya paundi 300,000 kwa wiki ili asaini mkataba mpya.
Habari toka England leo zinasema mazungumzo yameanza kutaka kumpa mkataba mpya mchezaji huyo ukizingatia mshahara anaoutaka na kama mpango huo utafanikiwa atakua ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi kwenye ligi hiyo.
Arsenal itafungua kampeni za ligi kuu msimu huu kwa kucheza dhidi ya mabingwa wa mwaka 2016 Leicester City mechi itakayochezwa usiku huu kwenye uwanja wa Emirates huku mchezaji huyo akikosekana kutokana na maumivu ya tumbo.
No comments