ARSENAL YATOKA PATUPU EUROPA LEAGUE
Safari ya Miaka 22 ya utawala wa kocha Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal umemalizika bila ya kombe lolote katika michuano ya Ulaya baada ya kutupwa nje katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Europa league wakifungwa bao 1-0 na Atletico Madrid.
Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Diego Costa ndiye aliyewaua Arsenal akifunga bao pekee katika mchezo huo wa marudiano dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza.
Bao hilo pekee limeifanya Atletico Madrid kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo ya pili Kwa u kubwa katika ngazi ya klabu barani Ulaya Kwa ushindi wa jumla wa bao 2-1 baada ya mechi ya awali kumalizika kwa sare ya bao 1-1 jijini London.
Arsene Wenger ambaye ameshatangaza kwamba ataihama klabu hiyo mwishoni wma msimu huu ataondoka Arsenal bila kombe lolote katika michuano ya Ulaya. Wengi wakitegemea pengine Wenger angeweza kuchukua kombe hili lakini mambo yakaenda kombo.
Katika mechi nyingine ya nusu fainali ya michuano hiyo Olympic Marseille imeweza kutinga hatua ya fainali licha ya kichapo cha bao 2-1 walichokipata ugenini dhidi ya RB Salzburg hivyo kutinga fainali kwa ushindi wa jumla wa goli 3-2 faida ya goli moja walilopata ugenini likiwaokoa.
No comments