BARCELONA YALIZWA NA REAL MADRID NYUMBANI, RONALDO KAFUNGA NA KUTOLEWA KWA KADI NYEKUNDU
Mechi ya kwanza ya Spanish Super Cup baina ya Wenyeji Barcelona na Real Madrid ilimalizika kwa Real Madrid kushinda bao 3-1.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Nou Camp ulishuhudia Real Madrid ikimaliza mchezo huo ikiwa pungufu baada ya Cristiano Ronaldo kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano baada ya kujiangusha wakati akitaka kwenda kufunga huku tayari akiwa na kadi ya njano aliyoipata alipofunga bao la kwanza na kuvua fulana yake.
Magoli mengine ya Real Madrid usiku wa jana yalifungwa na Gerard Pique aliyejifunga na Marco Asensio aliyefunga bao la tatu dakika ya mwisho ya mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji zaidi ya elfu 90.
Goli pekee la Barcelona lilifungwa kwa njia ya Penati na Lionel Messi ambaye alifunga baada ya Luis Suarez kuangushwa kwenye eneo la hatari.
No comments