NEYMAR AANZA KAZI VYEMA UFARANSA, AFANYA MAMBO YA "HATARI"
Mchezaji ghali zaidi kwasasa duniani Neymar jana usiku alianza vyema kuitumikia klabu yake ya PSG kwa kufunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa lingine katika ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Guingamp kwenye mchezo wa ligi kuu ya Ufaransa League one.
Neymar ambaye alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na PSG baada ya uhamisho wake toka Barcelona kukamilika alionekana kuwa mwiba kwa wapinzani wao huku Akileta muunganiko mzuri kwenye safu ya ushambuliaji yeye Di Maria na Cavani
Edison Cavani alifunga bao moja katika mabao hayo matatu huku bao lingine likifungwa na mlinzi wa Guingamp Jordan Ikoko.
No comments