HIZI NDIZO MECHI REAL MADRID WATAMKOSA RONALDO BAADA YA KUFUNGIWA.


Mshambuliaji wa Real Madrid  na mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo amefungiwa kucheza michezo mitano akiwa na Real Madrid baada ya kukutwa na hatia ya kumsukuma Refa kwenye mchezo wa jana dhidi ya Barcelona.

Katika mechi hiyo ya Super Cup ya Hispania baina ya  miamba hiyo kwenye dimba la Nou Camp Real Madrid iliibuka na ushindi wa bao 3-1 huku Ronaldo akifunga bao moja.

Tukio lililopelekea Ronaldo kukumbana na adhabu hiyo lilitokea dakika chache baada ya kufunga bao la pili la Real Madrid wakati akiwa katika harakati za kuongeza bao la tatu na kuangushwa na beki wa Barcelona Samwel Umtiti lakini jicho la mwamuzi liliona Ronaldo amejiangusha na ndipo kumpa kadi ya njano wakati akiwa tayari na kadi ya njano hivyo kutolewa nje kwa kadi nyekundu ndipo Ronaldo alipoonekana kukasirishwa na kumsukuma refa mgongoni.

Bado Ronaldo na Timu yake wanaweza kukata rufaa kwani wamepewa siku 10 kufanya hivyo lakini kama Rufaa hiyo itashindikana Ronaldo atapaswa sasa kukosa michezo ifuatayo:-

Barcelona (h) - Spanish Super Cup - 16 August
Deportivo La Coruna (a) - La Liga - 20 August
Valencia (h) - La Liga - 27 August
Levante (h) - La Liga - 9 September
Real Sociedad (a) La Liga - 17 September

No comments

Powered by Blogger.