BAADA YA NEYMAR SASA PSG WAMUIBUKIA MBAPPE WA MONACO


Wiki Moja baada ya kufanikiwa kumsajili Neymar kwa rekodi ya dunia paundi milioni 198,PSG wamehamia kwa Kylian Mbappe toka klabu ya Monaco ambao ni mabingwa wa Ufaransa.

Habari kutoka gazeti maarufu la michezo nchini Spain gazeti la Marca limeandika kwamba Kiasi cha paundi milioni 163 kimetajwa kwamba ndicho kilichotengwa na PSG kumpata kinda huyo raia wa Ufaransa ambaye aliwika vilivyo msimu uliopita.

Aidha taarifa zinasema kwamba Mbappe ameshauriwa na baba yake azitose Real Madrid na Barcelona na kusalia nchini Ufaransa katika uhamisho ambao utamfanya awe mchezaji wa pili ghali baada ya Neymar.

No comments

Powered by Blogger.