YANGA YACHUNA KUMTUMIA TIKETI YA NDEGE "MKATA UMEME" WA ZAMBIA

Dirisha la usajili huko Zambia linafungwa leo na mpaka sasa mustakabali wa Justine Zulu ndani ya kikosi cha Yanga haujulikani kwani kiungo huyo bado yuko nchini kwao akisubiri tiketi ya ndege kutoka Yanga wakati wenzake wakiendelea kujifua kambini Morogoro.

Hali hiyo inamfanya wakala wake Karin Nir kutishia kwamba iwapo Yanga wataenda kinyume na mkataba waliosaini na Zulu basi hawatosita kuwashtaki katika shirikisho la soka duniani, FIFA kuwadai fidia ya $100,000 ambayo ni zaidi ya Sh milioni milioni 200 za kitanzania.


Kumekua na tetesi kwamba Yanga wanataka kuvunja mkataba na 'mkata umeme' huyo ambao unapaswa kukamilika November mwaka huu kutokana na kuwa mbioni kumsajili kiungo raia wa Congo Kabamba Tshishimbi lakini jambo hilo limeonekana kama kaa la moto kwao.


Inasemekana kutokana na hali hiyo, Yanga wanafikiria kuendelea kuwa naye hadi pale atakapomaliza mkataba wake japo jambo hilo huenda likawatatiza katika nafasi za mastaa wa kigeni walio nao na wanaotaka kuwasajili.

No comments

Powered by Blogger.