BAADA YA KUPATA UNAHODHA MWANJALI AWAAHIDI SIMBA UBINGWA
Nahodha mpya wa timu ya soka ya Simba SC Ambao ni mabingwa wa Kombe la Shirikisho Nchini Tanzania na wawakilishi wa Kombe la Shirikisho barani Afrika Method Mwanjali amesema kwa sasa lengo lao ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom kama zawadi kwa mashabiki wao.
"Mashabiki wetu wameumia kwa muda mrefu sana kutokana na hali ya kutokuwa na makombe.Najua itakuwa ni safari ndefu na ngumu kwetu lakini mwisho wa msimu naahidi sisi tutakuwa mabingwa wa ligi kuu" Alisema Mchezaji huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns, Mpumhanga Aces na Caps United wakati alipoongea na mwandishi wetu moja kwa moja akiwa katika kambi ya Mazoezi Nchini Afrika Kusini.
Mwanjali ambae amewahi kuwa Nahodha wa timu ya Taifa ya Zimbabwe na Warriors FC alisema lengo lake jingine ni kuhakikisha timu yake inacheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kila mchezaji atimize jukumu lake akiwa uwanjani.
Simba inatarajia kurejea wiki hii ikitokea huko Afrika Kusini ambapo weekend hii inayokuja itakua ikitambulisha wachezaji wapya na jezi za msimu mpya watakapocheza na Rayon Sport ya Rwanda kwenye tamasha la SIMBA DAY.
No comments