WAARABU AKILI NYINGI NA HIVI NDIVYO WALIVYOPANGA KUMSAJILI NEYMAR NA KUEPUKA KUFUNGIWA NA UEFA
Moja kati ya habari inayoumiza Ulimwengu wa Wapenda Soka ni sakata la Uhamisho wa Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Barcelona Neymar ambaye inatajwa kwamba atasajiliwa na PSG ya Ufaransa katika dirisha hili la Usajili.
Kikubwa kinachozungumzwa ni jinsi gani PSG wataweza kutoa Paundi milioni 196 ambazo ndizo zilizoainishwa kwenye mkataba wa Neymar iwapo kuna timu itahitaji kumsajili na licha ya kutoa pesa hizo wasiweze kukumbana na rungu la Shirikisho la soka barani Ulaya kuhusu matumizi ya Pesa mchezoni (Financial Fair Play) ambayo inawabana PSG kutokana na mapato yao na matumizi.
www.wapendasoka.com kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari Duniani tunajaribu kuangalia namna ambayo PSG wataweza kuepuka hilo wakati huu ambao wao PSG wamekaa kimya kuepusha adhabu yoyote iwapo dili hili litafanikiwa.
Kwanza Mchezaji huyo kwa sasa yuko Nchini China akiiwakilisha klabu yake ya Barcelona kwenye Matangazo na taarifa zinasema akitoka China atatakiwa kupanda Ndege itakayopitia Qatar kisha kuelekea barani Ulaya
PSG inamilikiwa na kufadhiliwa na Kampuni ya Mafuta ya Qatar Investment Authority ambao wamejipanga kumpokea Neymar atakapotua nchini Qatar kumsainisha mkataba wa kuitangaza nchi hiyo kuelekea kwenye fainali za kombe la dunia mwaka 2022 zitakazopigwa huko mkataba unaokadiriwa kuwa na thamani ya Euro milioni 300 sawa na paundi milioni 265 ambazo ndizo Neymar atakazotumia kununua mkataba wake ili aondoke Barcelona
Kama Swala hilo litafanikiwa basi PSG hawataguswa na sheria hiyo kwani itakua ni Neymar mwenyewe ambaye ameamua kununua mkataba wake ili abaki Huru hivyo ataweza kujiunga na PSG kama Mchezaji huru kabisa
Haya yote yanakuja kutokana na mfululizo wa matukio yanayomhusisha mchezaji huyo kuondoka Barcelona na kama kweli atalazimisha kuondoka hiyo ndiyo njia pekee ya kuepuka adhabu kwa PSG lakini kama PSG wataamua kutoa pesa hizo kuwalipa Barcelona basi kitakachofata hapo PSG kumpata Neymar lakini kuzuiwa kucheza kwenye mashindano ya Ulaya na klabu pekee zinazoweza kulipa pesa hizo bila kupata adhabu ni Real Madrid na Manchester United.
No comments