USAJILI: YANGA YAMALIZANA NA RAPHAEL DAUDI WA MBEYA CITY

Mabingwa watetezi wa Ligi KuuVodacom Tanzania bara Yanga wamekamilisha usajili wa kiungo kinda na mahiri wa timu ya taifa, Taifa Stars kutoka Mbeya City ya jijini Mbeya, Raphael Daudi.


Kulikuwa na tetesi za muda mrefu juu ya Yanga kuvutiwa na Raphael ambaye alionesha kiwango kizuri katika ligi kuu msimu wa 2016/17 akiwa sambamba na mwenzake Kenny Ally ambaye ametimkia Singida United.

Hatimaye kiungo huyo amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Yanga na tayari ametua katika kambi ya timu hiyo iliyopo mkoani Morogoro kuungana na wenzake kuanzia leo.

Yanga wanaendelea na mazoezi yao mkoani humo kabla ya kurejea Dar es Salaam baadae wiki hii kwa ajili ya michezo ya kirafiki.

No comments

Powered by Blogger.