NGOMA AJIUNGA MAZOEZINI MOROGORO

Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma tayari amewasili kambini na kujiunga na wenzake huko Morogoro katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara na michuano ya kimataifa.

Ngoma aliwasili Jumamosi ya Julai 29 na Jumapili ya Julai 30 alisafiri hadi Morogoro ambako kikosi cha wanajangwani hao kimeweka kambi chini ya kocha mkuu George Lwandamina.

Yanga wanaendelea na mazoezi yao makali mkoani humo kabla ya kurejea Dar es Salaam baadae wiki hii kwa ajili ya michezo ya kirafiki.

No comments

Powered by Blogger.